Mbele ya waziri wa afya.. chuo kikuu cha Al-Ameed kimekuwa mwenyeji wa kongamano la wakuu wa vyuo vya udaktari vya Iraq.

Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimekuwa mwenyeji wa kongamano la wakuu wa vyuo vya udaktari vya Iraq.

Washiriki wa kongamano hilo wamejadili maendeleo ya kielimu katika sekta ya udaktari hapa Iraq, na namna ya kuboresha elimu na mazingira ya vyuo vya udaktari.

Katika kongamano hilo wamejadili viashiria vya mafanikio ya sekta ya udaktari na mambo mengine ya kisayansi.

Kongamano limehudhuriwa na waziri wa afya Dokta Swalehe Hasanawi, rais wa vyuo vya udaktari Dokta Anisi Khaliil Naail na wajumbe wa kamati ya wakuu wa vyuo vya udaktari vya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: