Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake imefanya kikao cha kwanza cha shindano la bibi Fedha.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kwanza cha shindano la Qur’ani la bibi Fedha awamu ya tato.

Mkuu wa kituo bibi Manaar Aljaburi amesema “Baada ya kuchuja washindani na kupata wenye sifa za kushiriki kwenye shindano hili, leo tumeanza kufanya kikao cha kwanza katika jengo la Maahadi lililopo mjini Najafu”.

Akabainisha kuwa “Shindano litadumu kwa muda wa siku mbili kwa kuendelea kuwasikiliza washiriki kutoka Najafu na kwenye vituo vya mikoa mingine”.

Mwisho wa shindano yatatangazwa majina ya washindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: