Shule za Dini Alkafeel upande wa wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zimemaliza mitihani ya nusu mwaka kwa msimu wa masomo 2022 – 2023.
Shule za Alkafeel katika mikoa yote ya Iraq, imefanya mitihani ya mwisho katika somo la Nahau, ambayo ni mitihani ya nusu mwaka.
Kamati ya usahihishaji wa mitihani inaendelea na kazi kwa lengo la kumaliza mapema na kutoa matokeo kwa muda uliopangwa.
Wanafunzi wameonyesha furaha kubwa kwa kufanya mitihani hiyo kwani matokeo yataonyesha juhudi zao, aidha wameshukuru kamati ya usimamizi wa mitihani kwa kazi nzuri.