Msafara mpya wa misaada kutoka Atabatu Abbasiyya umewasiri katika mji wa Ladhiqiyya “kitongoji cha Jiblah” kwa ajili ya kuendelea kutoa misaada ya kibinaadamu kwa waathirika wa tetemeko la ardhi.
Vitu vyote vimepelekwa moja kwa moja kwenye kituo cha Ataba kilichopo katika mji huo kwa ajili ya kuratibu shughuli na ugawaji wa misaada kwa familia za waathirika wa tetemeko la ardhi, na ugawaji wa vitu hivyo utaanza haraka iwezekanavyo.
Msafara wa kwanza ulikua unagawa zaidi ya vifurushi 2000 vya chakula kila siku katika mwezi wa pili kwa familia za waathirika katika mji wa Ladhiqiyya, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi.
Atabatu Abbasiyya tukufu ilituma msafara wa kwanza wa misaada nchini Sirya tarehe 22 mwezi wa pili, ulikuwa na zaidi ya tani (1555), ulikuwa umesheheni mahitaji muhimu kwa familia za waathirika ikiwa ni pamoja na hema kwa ajili ya watu waliopoteza nyumba zao kutokana na tetemeko hilo.