Mmoja wa wanafunzi wa Majmaa-Ilmi amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la wanafunzi wa shule za sekondari lililofanywa katika jiji la Bagdad.

Mmoja wa wanafunzi wa hifdhu katika Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu amekuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani ya shule za sekondari katika jiji la Bagdad.

Bwana Hassan Muhammad Abbasi kutoka Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa, amekuwa mshindi wa kwanza katika washindani (57) waliotoka mikoa tofauti, baada ya kuhifadhi kwa ubora mkubwa juzuu tatu za Qur’ani.

Washindi wa shindano hilo wamepewa zawadi sambamba na idara ya Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdadi.

Maahadi imekuwa ikishiriki kwenye mashindano tofauti ya usomaji wa Qur’ani, kwa lengo la kusambaza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya vizito viwili katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: