Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani katika mji wa Najafu, imetangaza kuthibiti kwa mwezi muandamo wa Ramadhani hivyo kesho siku ya Alkhamisi saw ana tarehe 23 Machi ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ofisi hiyo imesema kuwa “Imethibiti kuonekana mwezi muandamo wa Ramadhani kwa macho baada ya kuzama jua la siku ya Jumatano mwezi 29 Shabani katika maeneo tofauti ya Irad na nchi Jirani”.
Akaongeza kuwa “Hivyo kesho itakuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwafikishe sote kufanya mambo mema”.