Kitengo cha uboreshaji kinafanya semina ya kuhifadhi nahaju balagha kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinafanya semina ya kuhifadhi nahaju balagha kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mkufunzi wa semina Shekhe Haani Rabii amesema “Nahaju balagha inaumuhimu mkubwa baada ya Qur’ani na hadithi tukufu, ni kitabu chenye ufasaha na muongozo mtukufu”.

Akaongeza kuwa “Muhadhara umejikita katika kueleza ukamilifu wa nafsi na yanayohusu mwenendo wa mwanaadamu katika kuamiliana na wengine, kupitia usia wa Imamu Ali kwa mwanae Hassan (a.s) na ahadi yake kwa Maliku Ashtari (r.a), ikagusiwa pia hutuba ya Shaqshaqiyya na baadhi ya mambo muhimu”.

Semina imepata muitikio mkubwa kutoka kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, zinatarajiwa kufanywa semina zingine katika somo la nahaju balagha, kwa ajili ya kuendelea kuchota katika bahari ya elimu, kwa mujibu wa maelezo ya Rabii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: