Ugeni huo unatoa misaada ya aina tofauti, kuna misaada ya chakula, matibabu na mahitaji muhimu ya nyumbani.
Ugeni huo ulikuwa umeshatoa tani tatu za dawa na vifaa-tiba katika mji wa Swihah na Ladhiqiyya kwa ajili ya kusambazwa kwenye hospitali za miji hiyo, kwa lengo la kusaidia wananchi walioathirika na tetemeko katika sekta ya matibabu.
Jambo hili ni sehemu ya juhudi za utoaji wa misaada zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya kwa waathirika wa tetemeko nchini Sirya, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi.
Atabatu Abbasiyya ilituma msafara wa kwanza wa misaada nchini Sirya tarehe 22 mwezi wa pili, ulikuwa na zaidi ya tani (1555) za chakula na dawa, pamoja na hema kwa ajili ya watu walibomokewa na nyumba zao katika tetemeko hilo.