Majmaa-Ilmi imeanza vikao vya usomaji wa Qur’ani tukufu katika mwezi wa Ramadhani

Majmaa-Ilmi imeanza vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya Atabatu Abbasiyya katika mwezi wa Ramadhani.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Mkuu wa Maahadi Shekhe Jawadi Jasrawi amesema “Maahadi iliandaa ratiba kamili ya mwezi wa Ramadhani kabla ya kuanza kwa mwezi huu, kwa lengo la kunufaika na mwezi huu mtukufu”.

Akaongeza kuwa “Ratiba inavipengele vingi, Ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani tukufu kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abbasi saa kumi jioni”.

Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinarushwa na luninga kumi, kuna wasomi wa kitaifa na kimataifa wanaoshiriki usomaji wa Qur’ani kwenye vikao hivyo, jumla wa wasomaji 90 kutoka ndani ya Iraq watashiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: