Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake inafanya kikao cha kwanza cha usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani.

Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imefanya kikao cha kwanza cha usomaji wa Qur’ani tukufu.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaar Aljaburi amesema: “Maahadi imetenga muda wa kusoma Qur’ani tukufu kwa watumishi wake, kikao chake cha kwanza kimefanywa katika mji wa Najafu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa “Baada ya Qur’ani tukufu zilifuata tenzi na mashairi kutoka kikosi cha Nab’ul-Juud chini ya Maahadi, na mada ya kifiqhi kuhusu hukumu za funga kutoka kwa Zainabu Najaar”.

Maahadi haijaishia kufanya kikao vya usomaji katika ofisi zake peke yake, bali vikao hivyo vinafanywa kwenye vituo vyote vilivyopo katika mji wa Najafu na matawi yake huko mikoani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: