Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya kongamano la Qur’ani Nurain katika mwezi wa Ramadhani awamu ya pili kwenye mkoa wa Baabil.
Kongamano hilo linasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani ya Baabil chini ya Majmaa.
Mkuu wa Maahadi Sayyid Muntadhar Mashaikhi amesema kuwa “Kongamano linafanywa ndani ya mazaru ya Alawiyya-Sharifah (a.s) kwa kushirikiana na uongozi mkuu wa mazaru tukufu za kishia”.
Akaongeza kuwa “Kongamano linahusisha usomaji wa Qur’ani tukufu, mihadhara ya kielimu, nadwa na zitafuata ibada za Lailatul-Qadri”.
Akaendelea kusema “Kuna mashindano mengi ya Qur’ani na kielimu, aidha kunashindano la kuhifadhi hadithi arubaini za Ahlulbait (a.s) na hekina arubaini za kiongozi wa waumini (a.s)”.