Kitengo cha utumishi kimeanza kazi ya kusafisha maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya.

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza program kubwa ya kusafisha maeneo yanayozunguka haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na njia zinazo elekekea haram.

Kazi zimeanza baada ya usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa kuanzia na eneo la uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi kwenye vituo vya kutolea huduma ndani ya uzio wa Ataba na sehemu za kutunzia viatu, sehemu za kutunzia vitu na kwenye ngazi.

Barabara nyingi zinazo elekea Ataba tukufu zimesafishwa sambamba na maeneo yote yanayo zunguka haram takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: