Majmaa-Ilmi inafanya shindano la kwanza la usomaji wa Qur’ani kwa vikundi.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeanza vikao vya mashindano ya Qur’ani kwa vikundi ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mashindano hayo yanasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya chini ya Majmaa.

Kamati ya majaji inaongozwa na Shekhe Baasim Aabidi na Shekhe Jawadi Nasrawi katika (Hukumu na Tafsiri), Mula Ammaar Kinani katika (Hukumu na sauti), Ustadh Ali Bayati (Hukumu na Naghma) na Shekhe Maahir Hamiri katika (Hukumu na Hifdhu).

Kituo cha miradi ya Qur’ani chini ya Maahadi, kimeandaa maswali yatakayoulizwa kwenye mashindano, muulizaji atakuwa Sayyid Hasanaini Halo na Ustadhi Ali Faatwimi.

Shindano linavipengele vingi, kuna kipengele cha usomaji wa Qur’ani, tafsiri, kuhifadhi na hati, wapo washiriki kutoka sehemu tofauti, hata mazuwaru wanaokuwa ndani ya haram tukufu wanaruhusiwa kushiriki, kunamaswali maalum kwa ajili yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: