Kitengo cha habari na utamaduni kinaendesha program ya (Sufratul-Kafeel) katika mwezi wa Ramadhani kwenye nchi zaidi ya 11 barani Afrika.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinafanya program ya (Sufratul-Kafeel) kwenye nchi zaidi ya kumi na moja barani Afrika.

Program hiyo inasimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo hicho.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “(Sufratul-Kafeel) ni program inayoendeshwa na Markazi katika nchi zaidi ya kumi na moja barani Afrika, inahusisha kufanya majlisi, usomaji wa Qur’ani, kubainisha utukufu wa Ahlulbait (a.s) na nafasi yao katika Dini tukufu”.

Akaongeza kuwa “Kutakuwa na program maalum nchini Tanzania, inahusisha utoaji wa mihadhara ya Aqida, Qur’ani, Fiqhi sambama na kupika futari katika siku za kuadhimisha mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na maombolezo ya kifo cha kiongozi wa waumini (a.s)”.

Shimri akabainisha kuwa “Muwakilishi wa Markazi nchini Tanzania Shekhe Ammaar Hussein Maulid, alifanya program kubwa iliyohudhuriwa na wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), harakati zote zinafanywa chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: