Wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake wameshinda nafasi za kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani.

Wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya wamepata nafasi za kwanza kwenye kwenye mashindano ya Qur’ani.

Kiongozi wa Maahadi Ustadhat Manaar Aljaburi amesema “Tumefurahi sana kuwaona wanafunzi wetu wanapata nafasi za kwanza kwenye mashindano ya Qur’ani, yaliyosimamiwa na idara ya malezi katika mkoa wa Najafu”.

Akaongeza kuwa “Wanafunzi wa Maahadi (Huda Ihsaan, Rihana Ali Hashim na Sira Ra’adu Jaasim”, wameshinda nafasi tatu za mwanzo katika kikundi cha usomaji hatua ya mwanzo”.

Akaendelea kusema “Amma katika hatua ya upili mwanafunzi wa Maahadi bi (Maryam Ihsaan) amekuwa mshindi wa kwanza katika usomaji, jambo hili limetufurahisha sana kuona wanafunzi wetu wanapata ushindi kwenye sekta tofauti za usomaji wa Qur’ani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: