Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya, imeandaa ratiba ya usomaji wa Qur’ani tukufu katika mwezi wa Ramadhani.
Ratiba hiyo imeanza kutekelezwa toka siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani, miongoni mwa shule zinazoshiriki ni (Fakharu-Mukhadaraati, Nuuru Zaharaa, Daarul-Ilmi, Khadijatul-Kubra, Rihanatul-Mustwafa, Maasumatu-Sughra na Ummul-Banina -a.s-).
Ratiba hiyo inahusisha usomaji wa juzuu moja au mbili za Qur’ani kila siku, kujibu maswali ya Fiqhi na Aqidah sambamba na kutoa zawadi kwa washiriki wanaofanya vizuri.