Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya program ya Sufratul-Kafeel nchini Kamerun.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya program ya Sufratul-Kafeel katika nchi ya Kamerun ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Program hiyo inasimamiwa na Markazi Dirasaati Ifriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Program ya Sufratul-Kafeel inafanywa katika nchi nyingi barani Afrika, inamuitikio mkubwa kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), inahusisha kufanya vikao vya usomaji wa Qur’ani na kubainisha utukufu wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa “Muwakilishi wa Markazi katika nchi ya Kamerun Shekhe Muhammad Mukhtaar ametoa darsa ya Aqida na Qur’ani, yote hayo yanafanywa kwa kushirikiana na taasisi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Taasisi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) magharibi ya Kamerun inafanya program za mwezi mtukufu wa Ramadhani za kiibada kwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika maeneo ya Jirani na ofisi hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: