Katika Maqaam ya Imamu wa zama.. Majmaa-Ilmi imeanza kutekeleza ratiba ya usomaji wa Qur’ani

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani awamu ya tisa.

Ratiba hiyo inasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani chini ya Majmaa.

Kiongozi wa idara ya Tahfiidh katika Maahadi Shekhe Ali Rabii amesema “Usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi wa Ramadhani unafanywa katika Maqaam ya Imamu wa zama kwa mwaka wa tisa mfululizo, makumi ya watumishi wa Maqaam na mazuwaru wa ndani na nje ya Iraq wanashiriki”.

Akaongeza kuwa “Vikao kwa usomaji wa Qur’ani, vinalenga kufundisha washiriki usomaji sahihi na kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani tukufu”.

Makamo rais wa kitengo cha Maqaam Sayyid Haadi Mahadi Hanuun amesema “Kila siku baada ya swala ya Adhuhuri na Alasiri huwa tunasoma Qur’ani tukufu chini ya usimamizi wa Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kufundisha usomaji sahihi na kufanyia kazi mafundisho ya Qur’ani tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: