Sayyid Ali Muhammad amesema “Miongoni mwa kazi tunazofanya ni kudumisha usafi katika haram tukufu, kupuliza marashi, kuweka idadi kubwa ya misahafu, vitabu vya dua na ziara pamoja na turba za kutosha”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa majukumu ya kitengo kinachosimamia haram, ni kuongoza utembeaji wa mazuwaru ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuandaa sehemu za kuswalia”.
Kwa mujibu wa maelezo ya Muhammad “Watumishi wa kitengo hiki wanakazi nyingi, miongoni mwa kazi zao, ni kufanya usafi muda wote na kubadilisha mazulia kila inapohijatika”.