Sehemu ya ibada.. kitengo cha uboreshaji kinaendelea na ratiba ya mwezi wa Ramadhani

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na ratiba ya mwezi wa Ramadhani, inayohusisha utoaji wa elimu kwa watumishi na viongozi wa idara.

Rais wa kitengo Dokta Muhammad Hassan Jaabir amesema kuwa “Watumishi wa idara ya mafunzo wameandaa ratiba maalum kwa watumishi, sehemu ya ratiba hiyo inahusu vipengele vya ibada kama swala ya jamaa, usomaji wa Qur’ani tukufu na kuhudhuria mihadhara ya kidini”.

Kiongozi wa idara ya mafunzo Farasi Shimri amesema “Katika ratiba hii kunakipengele maalum kwa viongozi wa idara, wanafundishwa namna bora ya kusimamia watumishi katika vitengo vyao”.

Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu kinafanya semina nyingi za kujengea uwezo watumi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: