Kufuatia kuingia kwa msimu wa Rabii.. chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya maonyesho ya mimea ya mapambo.

Chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu kinafanya maonyesho ya mimea ya mapambo na mauwa, kufuatia kuingia kwa msimu wa Rabii.

Maonyesho hayo yanasimamiwa na idara ya kilimo katika chuo hicho.

Kiongozi wa idara ya uhandisi Ali Abdul-Jaliil amesema “Maonyesho yanafanywa ndani ya majengo ya chuo, sambamba na kuingia msimu wa Rabii, yataendelea kwa muda wa siku mbili, yanahusisha mauwa na mimea ya mapambo”.

Akaongeza kuwa “Maonyesho yanalenga kutambulisha wanafunzi na watumishi aina tofauti za mimea na majina yake sambamba na kueleza umuhimu wa kilimo na upandaji wa miti”.

Maonyesho hayo yamehusisha aina tofauti za mimea na miche inayouzwa kwa bei nafuu, pamoja na kuhamasisha kilimo na upandaji wa miti, aidha baadhi ya miche imetolewa bure kwa wakulima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: