Nchini Sirya.. ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya unafanya kikao cha kuomboleza kwa mzazi wa mmoja wa wajumbe wake.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya umefanya kikao cha taazia kwa mzazi wa mmoja wa wajumbe wake Sayyid Osama Salim Yusufu katika mkoa wa Laadhiqiyya nchini Sirya.

Kikao hicho kimefanywa kwenye makazi ya ugeni huo na kuhudhuriwa na waathirika wa tetembeko katika mkoa wa Laadhiqiyya nchini Sirya, miongoni mwa walioshiriki kwenye kikao hicho ni mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami na rais wa kitengo cha kutunza nidham katika Ataba tukufu Sayyid Hussein Shahrustani na mkuu wa kituo cha Multagal-Qamaru Shekhe Haarithi Daahi.

Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe waliopo katika mkoa wa Laadhiqiyya, na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na wapiganaji wa kikosi cha Abbasi, katika kikao hicho imesomwa Qur’ani tukufu na Shekhe Daahi akatoa mawaidha.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya ilituma ujumbe wa kutoa misaada ya kibinaadamu kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea nchini Sirya na kusababisha hasara kubwa, msafara huo unatekeleza majukumu yake chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: