Nchini Kenya.. kitengo cha Habari na utamaduni chafanya program ya (Sufratul-Kafeel) ya mwezi wa Ramadhani.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinafanya program ya (Sufratul-Kafeel) ya mwezi wa Ramadhani katika mji wa Mombasa nchini Kenya.

Program hiyo inatekelezwa kwenye nchi kumi na moja za Afrika chini ya Markazi Dirasaati Afriqiyya.

Mkuu wa Markazi Shekhe Sataar Saadi Shimri amesema “Program hiyo inabainisha utukufu wa mwezi wa Ramadhani na kufanya ibada maalu za mwezi huu kwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka miji tofauti”.

Akaongeza kuwa “Program hiyo ilikuwa na vikao viwili, cha kwanza kabla ya futari ambapo wameelezwa utukufu wa mwezi wa Ramadhani na umuhimu wa ibada ya funga kiroho na kiafya, na kikao cha pili baada ya futari, ambapo zimesomwa dua zilizopokewa kutoka kwa Ahlulbait (a.s) ikiwemo dua ya Iftitaah”.

Akabainisha kuwa “Muwakilishi wa Markazi katika nchi ya Kenya Shekhe Ammaar Ali anasimamia utekelezaji wa ratiba hiyo” akafafanua kuwa “Program hii ni sehemu ya harakati za kidini na kimaadili kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika bara la Afrika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: