Kiongozi wa idara bibi Adhraa Shami amesema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani katika mwezi wa Ramadhani vinafanywa ndani ya Maqaamu ya Imamu wa zama (a.s) kila siku, chini ya ratiba maalum”.
Akabainisha kuwa “Mwaka huu kunavipengele vingi vilivyo ongezwa kwenye usomaji wa Qur’ani, kunamasomo ya Fiqhi yanayo husisha hukumu za funga, ufafanuzi wa baadhi ya hukumu zinazohusu wanawake katika Maisha yao ya kila siku, pamoja na somo la tafsiri ya Qur’ani”.
Akaendelea kusema “Vikao vya usomaji wa Qur’ani vinapata mwitikio mkubwa kutoka kwa waumini na mazuwaru watukufu”.