Katika hospitali ya Alkafeel.. umefanywa uonganishaji wa mifupa tofauti ya uso wa kijana iliyo vunjika kwenye ajali.

Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kuunganisha mifupa ya uso na mikono ya kijana iliyokuwa imevunjika kwenye ajali ya gari.

Daktari bingwa wa uso na mikono katika hospitali hiyo Dokta Muammar A’araji amesema, ajali ya gari ilisababisha kuvunjika mifupa ya uso na mikono ya kijana huyo.

Akaongeza kuwa, baada ya kumfanyia vipimo na kumuingiza mgonjwa kwenye chumba cha upasuaji, tulianza kazi ya kuunganisha mifupa ya uso na kuweka meno ya bandia sehemu ambazo meno yake yametoka.

Katika upasuaji huo tumetumia vifaa-tiba vya kisasa, kazi hiyo ilidumu kwa muda wa saa tatu, na iliisha kwa mafanikio makubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: