Kitengo cha habari kinafanya program ya Sufratul-Kafeel katika nchi ya Benin.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kinafanya program ya Sufratul-Kafeel katika mji wa Barako kitongoji cha Buruju kaskazini ya nchi ya Benin.

Program hiyo inaendeshwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.

Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Markazi inafanya program za Sufratul-Kafeel katika nchi kumi na moja za Afrika, katika nchi ya Benin program hiyo inafanywa chini ya usimamizi wa muwakilishi wa Markazi Shekhe Hassan Omidi na kuhudhuliwa na kundi kubwa la wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mji huo”.

Akaongeza kuwa “Siku za nyuma Shekhe Ismail Abda na shekhe Saidi Mikaeli walifanya progam maalum ya usomaji wa dua za mwezi wa Ramadhani huku Shekhe Suleiman akitoa muhadhara kwa lugha yao, akabainisha sababu za kuja kwa mitume watukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: