Majmaa-Ilmi imehitimisha shindano la Qur’ani awamu ya sita katika mji wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imehitimisha shindano la Qur’ani awamu ya sita katika mkoa wa Baabil.

Shindano limesimamiwa na Maahadi ya Qur’ani ya Baabil chini ya Majmaa.

Rais wa Majmaa Dokta Mushtaqu Ali amesema “Shindano la Qur’ani tukufu lililokuwa sehemu ya ratiba ya kongamano la Nurain, linahusisha utoaji wa mihadhara ya kielimu, mashindano ya Qur’ani na usomaji wa Qur’ani, limehitimishwa”.

Akaongeza kuwa “Kikosi cha Mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi-Atwaasha Karbalaa), kimepata nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya vikundi”.

Makamo wa kiongozi mkuu wa kitengo cha utamaduni katika mazaru ya Alawiyya Sharifa (a.s) Shekhe Hassan Silawi amesema “Tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Maahadi katika kongamano hili tukufu”.

Akaongeza kuwa, kongamano lilikuwa na mambo mengi muhimu kwa vijana na Dini tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: