Atabatu Abbasiyya inaendesha shindano la mjukuu mkubwa (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza kufanyika kwa shindano la (mjukuu mkubwa) kufuatia kukaribia kwa kumbukumbu ya kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Shindano limefanywa pembezoni mwa kongamano la kuzaliwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kwa muda wa siku tatu, kuanzia siku ya Jumapili tarehe (2/4/2023m).

Majina kumi ya washindi yatatangazwa siku ya Jumanne jioni (4/4/2023m), juu ya jukwaa la Atabatu Abbasiyya tukufu, zawadi ya washindi itakuwa dinari (100,000) za Iraq kwa kila mmoja.

Ili mshindi aweze kupewa zawadi yake anatakiwa awepo kwenye hafla itakayo fanyika siku ya Jumatano tarehe (5/4/2023m), katika Husseiniyya ya Ibun Idrisa Alhilly (r.a) iliyopo katika mji wa Baabil saa mbili jioni.

Iwapo mshindi atapata udhuru na kushindwa kufika kwenye hafla hiyo, ataenda kuchua zawadi yake kwenye ofisi za kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu siku tatu baada ya kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: