Makumusho ya Alkafeel imeandaa semina ya kuwajengea uwezo wahudumu wa kitengo cha usimamizi wa haram.

Kitengo cha makumbusho katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeandaa semina ya kuwajengea uwezo wahudumu wa kitengo cha kusimamia haram kuhusu namna ya kutengeneza miswala.

Semina imejikita katika ufundishaji wa kutengeneza miswala kwa mikono na mitambo, wanafundishwa kutengeneza miswala kwa njia ya kutumia mikono (asili) na kwa njia ya kutumia mtambo maalum unaoitwa (Shiraza).

Aidha wamefundishwa namna ya kutambua mswala uliotengenezwa kwa mikono na uliotengenezwa kwa mashine, sambamba na namna ya kupanga nyuzi kutokana na aina ya mswala unaotengenezwa.

Mwisho wa semina hiyo vikatolewa vyeti vya ushiriki kwa kila aliyeshiriki kwenye semina hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: