Tawi la Majmaa-Ilmi kwenye maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa yanayofanyika jijini Tehran limepata mwitikio mkubwa.

Tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya linaloshiriki katika maonyesho ya Qur’ani ya kimataifa jijini Tehran limepata mwitikio mkubwa.

Rais wa ugeni wa Majmaa Shekhe Mahadi Qalandari Abayati amesema “Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inafanya juhudi za kujulisha ulimwengu wa kiislamu mambo yanayopatikana katika vituo vyake, ikiwa ni pamoja na uchapishaji wa misahafu, vitabu vya tafsiri na maarifa ya Qur’ani”.

Akaongeza kuwa “Waziri wa utamaduni wa Iran na baadhi ya viongozi wa kitaifa wametembelea tawi la Majmaa na kuangalia machapisho yanayotolewa na tawi hilo”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Shekhe Abayati, watu waliotembelea tawi hilo wamepongeza huduma zinazotolewa katika kuhudumia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: