Atabatu Abbasiyya imetangaza majina ya waliofaulu kwenye shindano la mjukuu mkubwa (a.s).

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umetangaza majina ya waliofaulu kwenye shindano la (mjukuu mkubwa -a.s-) lililofanywa pembezoni mwa kongamano la kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Washindi wanatakiwa kuhudhuria kwenye hafla itakayofanywa Jumatano (5/4/2023m) huko Baabil saa (2:00) jioni, katika Husseiniyya ya Ibun Idrisa Alhilly (r.a).

Kama mshindi atakuwa na udhuru wa kutofika kwenye hafla hiyo, itamlazimu aende kwenye ofisi za kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kuanzia baada ya hafla hiyo hadi mwisho wa mwezi huu wa nne.

Akasema kuwa zawadi itakayotolewa kwa kila mshindi ni dinari (100,000) za kiiraq, watapewa zayadi hiyo washindi kumi wa mwanzo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: