Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kinaadhimisha mazazi ya Imamu Hassan (a.s).

Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu kimeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wa Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Kufanya hivyo ni sehemu ya utamaduni wake kila mwaka wa kuadhimisha tarehe walizozaliwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na kuomboleza tarehe walizokufa, hivyo wameandaa ratiba ya kuadhimisha mazazi hayo kwa kufanya kongamano la waimba mashairi na kuhudhuriwa na mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya mazingira ya shangwe na furaha.

Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na imehudhuriwa na mazuwaru wengi wakiwemo waimbaji na washairi waliopamba hafla hiyo kwa qaswida na mashairi ya kuwasifu Ahlulbait (a.s) pamoja na kuisifu nchi yetu kipenzi ya Iraq.

Aidha hafla imepambwa na dua za kuombea amani na utulivu taifa la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: