Haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inasafishwa muda wote.

Wahudumu wa idara ya kusimamia haram ya Atabatu Abbasiyya wanasafisha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) muda wote.

Kingozi wa idara ya kusimamia haram Sayyid Nizaar Ghina Khaliil amesema “Watumushi wa idara yetu wanafanya usafi ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) muda wote, usafi huo unahusisha, kupiga deki, kusafisha kuta, milango, madirisha kwa kutumia vitu ambavyo ni rafiki kwa mazingira”.

Akaongeza kuwa “Tunafanya usafi kwa kufuata ratiba maalum, tunatumia zaidi nyakati ambazo mazuwaru hupungua, ili kuepusha usumbufu wakati wa kufanya ziara, sambamba na kutumia vifaa maalum ambavyo vinasaidia kutunza vitu vilivyomo ndani ya haram tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: