Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya anakagua huduma zinazotolewa kwa mazuwaru.

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, amekagua huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Mheshimiwa katibu mkuu amefuatana na kiongozi mtendaji wa ofisi yake na rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Muhammad Ali Azhar.

Wametembelea uwanja wa Ummul-Banina (a.s) kuangalia kazi inayoendelea sehemu hiyo na huduma zinazotolewa na wahudumu wa kitongo cha utumishi, halafu wakaenda kwenye kitengo cha mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ziara hiyo ni sehemu ya ratiba ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuangalia utendaji kazi wa wahudumu wa Ataba katika mwezi wa Ramadhani sambamba na ongezeko la mazuwaru wanaokuja katika eneo hili ndani ya mwezi mtukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuhudumia mazuwaru katika mwezi wa Ramadhani, na kufanya ibada za ziara na dua, ratiba inavipengele vingi ikiwa ni pamoja na usomaji wa Qur’ani na utoaji wa mihadhara ya Dini kila siku kwa nyakati tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: