Sayyid Swafi asisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya walimu na wanafunzi.

Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amesisitiza umuhimu wa kuboresha mazingira ya walimu na wanafunzi.

Ameyasema hayo alipotembelea kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amesifu harakati zinazofanywa na idara ya shule na watumishi wake sambamba na mikakati ya elimu iliyowekwa, inayoendana na maendeleo ya kisasa katika sekta ya malezi na elimu ya juu.

Mheshimiwa amepokewa na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Hassan Daakhil Hasanawi.

Akahimiza umuhimu wa kuboresha mazingira kwa wote na kusaidia walezi na walimu waweze kutekeleza majukumu yao kwa urahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: