Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kupitia Markazi Dirasaati Afriqiyya, kimefanya program ya (Sufratul-Kafeel) kwenye nchi kumi na moja za Afrika.
Mkuu wa Markazi Shekhe Saadi Sataar Shimri amesema “Program imeandaa futari ya pamoja katika kumbukumbu ya mazazi ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na utoaji wa mihadhara ya kueleza historia yake na nafasi aliyonayo kwa waimini”.
Akasema kuwa “Nchi zinazofanya program hiyo ni Laiberia, Tanzania, Kenya, Gana, Madagaska, Kamerun, Senegal, Mauritania, Naijeria, Seralion na Benin”.
Akabainisha kuwa “Program inahusisha usomaji wa Qur’ani, dua maalum za mwezi wa Ramadhani na utoaji wa mihadhara, ratiba hiyo ni ya mwezi mzima wa Ramadhani kama ilivyo pangwa na Markazi kwa nchi hizo za Afrika.