Katika machapisho yaliyovutia watu wengi ni misahafu iliyo chapishwa na Majmaa, kulikuwa na aina sita za misahafu yenye ukubwa tofauti, iliyoandikwa kwa hati za kiiraq na kuwekwa mapambo ya kiiraq, misahafu hiyo ilichapishwa na kituo cha uchapaji cha Atabatu Abbasiyya.
Machapisho ya Qur’ani kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu yamepata heshima maalum kwenye maonyesho ya kimataifa ya thelathini nchini Iran, yametembelewa na watu wengi sana wakiwemo viongozi wa kidini na kijamii.