Majmaa-Ilmi na kitengo cha Habari wanajiandaa kuanza ratiba maalum ya kiibada katika kuhuisha siku za Lailatul-Qadri.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu na kitengo cha Habari wamekamilisha maandalizi ya kuhuisha siku za Lailatul-Qadri.

Rais wa Majmaa-Ilmi Dokta Mushtaqu Ali amesema kuwa Atabatu Abbasiyya inatilia umuhimu mkubwa swala la kuhuisha siku za Lailatul-Qadri ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kufanya ibada maalum ndani ya siku hizo kuanzia saa kumi jioni hadi saa sita usiku katika siku zote za Lailatul-Qadri.

Akaongeza kuwa, hakika kitengo cha Majmaa-Ilmi kwa kushitikiana na kitengo cha Habari, kitengo cha miradi ya kihandisi idara ya vipaza sauti, kitengo cha usimamizi wa haram, wanafanya maandalizi ya kuhuisha siku hizo tukufu kwa kufanya ibada mbalimbali pamoja na kusoma Qur’ani na dua.

Akasema kuwa sehemu iliyoteuliwa kwa ajili ya ibada hizo haijawahi kushuhudia harakati za mazuwaru.

Kitengo cha habari kitarusha ibada zitakazo fanywa hapo moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vitakavyopenda kurusha matangazo hayo.

Tunatarajia idadi kubwa ya watumishi wa Majmaa-Ilmi na vitengo vingine vya Ataba pamoja na mazuwaru watukufu watashiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: