Kitengo cha kusimamia haram kimeweka vitambaa vinavyo ashiria huzuni.

Kitengo cha kusimamia haram katika Atabatu Abbasiyya, kimeweka vitambaa vinavyo ashiria huzuni kama sehemu ya maandalizi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Makamo rais wa kitengo hicho Shekhe Zainul-Aabidina Kuraishi amesema “Wahudumu wetu wameanza kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni kwenye korido za Atabatu Abbasiyya ndani na nje, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Akaongeza kuwa “Tumeandaa mapambo ya kila tukio la kidini na vitambaa maalum kwa mnasaba wa Ahlulbait (a.s), huwekwa ndani na nje ya haram kwenye kila mnasaba, ukiwemo mnasaba huu wa kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s)”.

Akafafanua kuwa “Wahudumu wa idara ya taa, wamefunga taa zenye mwanga mwekundu zinazo endana na tukio la msiba” akasema: “Kuna ratiba nyingine ya usomaji wa Qur’ani na ufungaji wa taa maalum sambamba na kuandika maneno yanayo ashiria huzuni katika eneo la usomaji wa Qur’ani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: