Ofisi ya Sayyid Sistani imetoa wito wa kufuta jina ya Marjaa Dini mkuu kwenye Muswala uliofunguliwa na shule ya (Daarul-Ilmi) katika mji wa Najafu.

Ofisi ya Sayyid Sistani imetoa wito wa kufuta jina la Marjaa Dini mkuu kwenye muswala uliofunguliwa hivi karibuni katika shule ya (Daarul-Ilmi) katika mji wa Najafu, kupitia tamko alilotumiwa Sayyid Jawaad Khui mkuu wa Shule.

Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

Mheshimiwa Allaamah Sayyid Jawaad Khui kiongozi mkuu wa shule ya Daarul-Ilmi ya Imamu Khui.

Amani ya Mwenyezi Mungu na baraka zake ziwe juu yenu.

Tumeshangazwa na kilichotangazwa wakati wa ufunguzi wa muswala wa shule ya (Daarul-Ilmi) kwa kuipa jina la Mheshimiwa Sayyid Sistani, ni wazi kuwa mmefanya hivyo kwa lengo la kuonyesha heshima kwa Marjaa Dini mkuu na kumjulisha kuhusu ukamilishaji wa jingo la bweni la shule hiyo, na hilo ni jambo zuri.

Lakini Mheshimiwa hafurahishwi na kuandikwa jina lake sehemu yeyote ya umma, yeye mwenyewe amekuwa akiandika majina ya wanachuoni wengine -kama Najmu-Aimah, Alaamh Albalaghi, Mhakiki Shekhe Hussein- unatakiwa kubadilisha jina uliloandika, tunatanguliza shukrani za dhati kwako.

Ofisi ya Sayyid Sistani – Najafu Ashrafu.

Mwezi wa Ramadhani 17 - 1444h.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: