Mbele ya malalo za watoto wake.. yamefanyika matembezi ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Mawakibu za Karbala zimefanya matembezi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), mbele ya malalo za watoto wake Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi hayo ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Karbala, katika tukio hili na mengine ya kuomboleza tarehe za kufariki kwa Maimamu watakasifu (a.s).

Sayyid Ahmadi Fatwimi mmoja wa wahudumu wa maukibu amesema “Mawakibu za Karbala katika tukio hili hugawa futari kila mwaka na hufanya matembezi ya kuomboleza kuelekea katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa, mawakibu hutoa huduma kwa mazuwaru na kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s) sambamba na kutoa pole kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: