Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s).

Atabatu Abbasiyya imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) na kuhudhuriwa na watumishi wa malalo takatifu.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyofuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Raafid Rashidi, ameongea kuhusu historia ya Imamu Ali (a.s), ushujaa, ufasaha na namna alivyojitolea katika uislamu.

Majlisi zitaendelea kwa muda wa siku tatu ndani ya ukumi wa utawala, kuanzia siku aliyojeruhiwa kiongozi wa waumini (a.s) hadi siku aliyofariki.

Kuta za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zimewekwa mapambo meusi na mabango yenye jumbe za huzuni, aidha zimefungwa taa nyekundu kama sehemu ya kuonyesha huzuni na majonzi kutokana na msiba huu mkubwa mbele ya Mtume na Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: