Chuo kikuu cha Alkafeel kinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s).

Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini (a.s).

Majlisi imehudhuriwa na rais wa chuo Dokta Nuris Shahidi Dahani na msaidizi wa kitenge cha taaluma Dokta Nawaal Aaid Almayali, wakuu wa wavitivo, wahadhiri na watumishi wa chuo.

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Zubaidi, kisha Shekhe Jaasim Afdhalu akapanda kwenye mimbari na kuongea kuhusu historia ya kiongozi wa waumini (a.s) na utukufu wake.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi na qaswida za kuomboleza, zilizo amsha hisi za majonzi na huzuni katika nyoyo za waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: