Mkuu wa Majmaa ya kujenga ukaribu baina ya madhehebu za kiislamu amepongeza mafanikio ya Majmaa-Ilmi katika maonyesho ya Tehran.

Kiongozi mkuu wa Majmaa ya kujenga ukaribu baina ya madhehebu za kiislamu Dokta Hamidi Shahriyari, amepongeza mafanikio ya Majmaa-Ilmi katika maonyesho ya kimataifa yaliyofanyika Tehran.

Ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya katika maonyesho ya kimataifa yaliyofanyika Tehran awamu ya thelathini.

Ugeni huo umepokewa na rais wa Majmaa-Ilmi katika mji mkuu wa Tehran Shekhe Mahadi Qalandari Albayati.

Shahriyari amepongeza mpangilio na utendaji wa Majmaa-Ilmi, amesifu ubora wa vitabu vya aina mbalimbali wanavyo chapisha, vikiwemo vitabu vya kitafiti, kitamaduni, maarifa ya Qur’ani na tafsiri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: