Majmaa-Ilmi inafanya semina kuhusu maandishi ya msahafu na hati zake.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya semina kuhusu maandishi ya msahafu, hati, na mapambo yake.

Semina imesimamiwa na kituo cha uandishi wa msahafu chini ya Majmaa.

Mkuu wa kituo na muwezeshaji wa semina hiyo Shekhe Dhiyaau-Dini Zubaidi amesema: “Senina inalenga kutambulisha kitabu cha Mwenyezi Mungu na kufafanua historia ya misahafu na hati zake, akasema kuwa semina hiyo imefanywa ndani ya Sardabu ya mkono mtukufu katika Atabatu Abbasiyya”.

Akaongeza kuwa “Semina imehudhuruwa na watumishi wengi wa kitengo cha Habari na utamaduni pamoja na wawakilishi wa vituo vya uandishi wa misahafu, Sayyid Karaar Mussawi ameeleza historia ya hati za misahafu na hatua za uboreshwaji wake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: