Watumishi wa Ataba mbili wanaomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s).

Watumishi wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, wameomboleza kifo cha Imamu Ali (a.s) kupitia maukibu ya uombolezaji ya pamoja.

Matembezi ya maukibu yameanzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia uwanja wa katikati ya haram mbili huku wanaimba kaswida za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni katika nyoyo za waumini na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).

Baada ya kuwasili katika haram ya Imamu Hussein (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza kwa ushiriki wa mazuwaru wengi, hapo zikasomwa tenzi na kaswida zilizoeleza maisha na historia ya Imamu Ali (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: