Kitengo cha habari na utamaduni kinafanya nadwa ya kitamaduni katika mkoa wa Dhiqaar.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya nadwa iliyo jikita katika mada mbili ambazo ni (Binaadamu wapo makundi mawili) na (Nafasi ya Imamu Ali -a.s- katika Raja’a) mkoani Dhiqaar.

Nadwa imefanywa chini ya usimamizi wa kituo cha Multaqal-Qamaru tawi la Dhiqaar, kwa kushirikiana na taasisi ya Nurul-Imamu Hussein (a.s) ndani ya Husseiniyya ya Arubaini katika kitongoji cha Al-Awiyah.

Mhadhiri wa nadwa hiyo alikuwa ni Shekhe Akram Atabi, akaeleza kauli ya Imamu Ali (a.s) ya kugawa watu makundi mawili, na akafafanua kila kindi, sambamba na kueleza nafasi ya Imamu Ali katika kudhihiri Imamu Mahadi (a.f).

Washiriki wameuliza maswali na kupewa majibu, hali kadhalika zimetajwa harakati zinazofanywa na kituo hicho pamoja na malengo yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: