Makamo rais wa kitengo hicho Mhandisi Abbasi Ali amesema “Baada ya kimbunga na mvua ya jana siku ya Jumatano, watumishi wetu leo asubuhi wameanza kazi ya kusafisha jengo takatifu na maeneo yeto yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Akaongeza kuwa “Kazi ya usafi imehusisha barabara zinazozunguka malalo takatifu”.
Akafafanua kuwa “Wahudumu wetu walianza kusafisha eneo la mlango wa Qibla kwa kutumia vifaa mbalimbali, wakaendelea kusafisha na maeneo mengine”.