Tawi la Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya limefanya hafla ya usomaji wa Qur’ani katika maonyesho ya Tehran ya kimataifa.
Msomaji wa Majmaa na mmoja wa wanafunzi wa Hauza Shekhe Mahadi Qalandari Albayati amesoma Qur’ani kwa mahadhi ya Kiiraq ya huzuni.
Katika hafla hiyo, yametangazwa majina ya washindi wa zawadi ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyotumika kwenye maonyesho hayo na zawadi zingine za kutabaruku.
Ushiriki wa Majmaa kwenye maonyesho ya Tehran ya kimataifa ni sehemu ya harakati zake.