Kitengo cha mgahawa kimesema: Zaidi ya watu laki moja na elfu hamsini wamenufaika na huduma zetu katika siku za Lailatul-Qadri.

Kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya kimesema kuwa zaidi ya watu (150,000) wamenufaika na huduma ya chakula katika siku za Lailatul-Qadri.

Rais wa kitengo cha mgahawa Sayyid Aadil Jafari amesema “Idadi ya mazuwaru inaongezeka kila siku katika mji wa Karbala ndani ya siku hizi la Lailatul-Qadri, watu wanakuja kumtembelea Imamu Hussein na ndugu yake Abulafadhil Abbasi (a.s), jambo hilo linasababisha na sisi kuongeza huduma katika mgahawa (mudhifu) wetu.

Akaongeza kuwa: “Ndani ya siku tatu za Lailatul-Qadri, mgahawa umegawa zaidi ya sahani za chakula (150,000) sambamba na ugawaji wa maji ya kunywa, juisi, matunda na vitafunwa”.

Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya hutoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja kumtembelea Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mwaka mzima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: